Friday, August 29, 2014

WASTARA JUMA AZICHAPA NA MUMEWE MAHAKAMANI



WIKI iliyopita katika makala haya tuliishia pale mwigizaji Wastara Juma alivyokimbizwa na mumewe wa kwanza na kuokolewa na difenda la polisi, TUENDELEE…



APEWA TALAKA

Mwandishi: Nini kiliendelea baada ya purukushani hizo zote?
“Zilipita siku tatu mume wangu alinipigia simu akiwa na dada yake na kunitamkia kwamba ameniacha kwa talaka tatu na huyo dada yake ndiye shahidi na hiyo ilikuwa mwaka 1999.
“Haikupita miezi miwili alikuja nyumbani na kuandika talaka tatu za maandishi hivyo nikawa nipo tu nyumbani na wakati misukosuko yote ikiendelea, mama yangu alikuwa ameshafariki.

WASULUHISHWA
Mwandishi: Kwa hiyo katika kupewa talaka hizo hamkurudiana tena?
“Baada ya kunipa talaka kwenye simu wazazi wake walikuja kusuluhisha tukarudiana akaja kumchukua mtoto na akaenda kukaa naye Zanzibar huku mimi nikiwa nimepata kazi ambapo mwanangu alikaa huko kwa mwaka mmoja nilipoenda kumuona nikakuta ana utapia mlo ukweli nilisikia uchungu, niliwaambia namchukua mwanangu akanipokonya na kwenda kujifungia naye chumbani ambako nilienda na kuvunja mlango nikamchukua mtoto kwa nguvu ndipo alipokaa kwa miezi miwili akaja kuniandikia talaka ya maandishi.

APATA MCHUMBA MWINGINE
Mwandishi: Je baada ya kupewa talaka ulipata mchumba mwingine?

“Ndiyo nilipata mchumba ambaye kwa upande mwingine ni ndugu yetu ambaye alikuwa anaishi hukohuko Zanzibar lakini nilishangaa siku moja nikiwa naye pamoja na ndugu zangu wengine tumetoka kutembea, tulipofika nyumbani polisi wakaingia na kutuulizia mimi na yule mchumba ambapo walituchukua mpaka kituoni na nilipohoji walisema kwamba mume huyo wa zamani amenifuma na mwanaume mwingine wakati yeye ndiye mume wangu.


Wastara Juma akipozi.
“Tulikaa selo mpaka familia zote mbili zilipokuja na kuzungumza lakini hawakufikia muafaka, nikaomba ile kesi ipelekwe mahakamani kwa sababu sikuwa mke wa mtu, tukaenda mahakamani yule kijana ambaye ndiyo tulikuwa tunaanza uchumba yeye hakuwa na makosa tukabaki mimi na huyo mwanaume.

“Ilikuwa ni kama sinema kwani kila tulipokuwa tukikutana mahakamani tulikuwa tunapigana sana mpaka mahakama ikaamua kutuhamishia kwenye mahakama ya Kadhi (inayoshughulika na masuala ya ndoa) ambapo mwanaume huyo alidai kwamba anataka arudishiwe mahari yake nikaomba kesi ihamishiwe Dar, nikakubaliwa.

“Kabla sijafika Dar nikakuta ameshaniwahi na kwenda BAKWATA ambako alitakiwa anipe talaka lakini akaandika majina tu na kuondoka, Bakwata walinisaidia tukapeleka mahakamani ambapo tangazo la mahakama kutoa talaka lilitangazwa kwenye magazeti ya serikali kwa siku 39 ili mwenye pingamizi apeleke lakini hakuna aliyejitokeza hivyo nikapewa talaka na mahakama.

Mwandishi: Baada ya kumalizana na mumeo huyo uliendelea tena na yule mchumba?


“Niliendelea naye lakini tukiwa kwenye kuchunguzana siku moja nilikwenda kumtembelea kwao akaja mwanamke akawa anazungumza maneno mengi yakimhusu huyo mchumba kumbe alikuwa ni mwanamke wake, alipoondoka huyo jioni yake akaja mwingine akiwa anamuulizia na kesho yake akaja wa tatu ambaye alikuwa akilalamika kwamba huyo mwanaume anasikia ana mchumba wakati yeye ni mwanamke wake.


0 comments:

Post a Comment