Sunday, August 31, 2014

UVIVU WAKO NI SABABU YA MWENZIO KUCHEPUKA...soma full story hapa


Kuna watu ambao wamekuwa hodari kujisifu kuwa wao hutoa unyumba kwa ‘kibaba’. Yaani huwapimia wenzi wao. Kwa mitazamo yao, hujiona wapo sahihi. Tabia hii ipo kwa wanawake zaidi, japo kuna wanaume ambao nao ni wagumu kutekeleza mahitaji ya wapenzi wao.Hata hivyo, kuna kitu cha kuweka sawa hapa; Wakati mwanamke anapobana ‘staftahi’ kwa mwenzake, huhesabika ni mchoyo! Kwa mwanaume yeye huonekana ni goigoi. Kwamba mambo hayawezi ndiyo maana hatekelezi shughuli. Ataambiwa ana tatizo la zile nguvu zetu!

Mwanamke anaweza kujisifu hata kwa wenzake. Akiwa kwenye vikao vya kusukana au katika soga nyingine, atajimwagia sifa tele kwamba yeye inaweza kupita miezi bila kuingia uwanjani na mwenzi wake. Hili, linawafanya wanaume wengi wateseke na matokeo yake hutafuta tiba mbadala.


Mwanaume hawezi kujisifu kwa marafiki zake kuwa yeye huwa akisumbuliwa na mwenzi wake, humpa mgongo! Ni wazi akisema hivyo atachekwa. Yaani mwanamke kugomea kutoa unyumba ni ushujaa wakati mwanaume akikataa, atachukuliwa kwamba ana tatizo la kiafya! Dhana hii sikubaliani nayo, kwa hiyo nahitaji kutoa shule!Kwangu mimi, kila aliye mvivu wa kuingia shughulini ana tatizo! Kwa mwanaume na mwanamke, wote wana kasoro ya nguvu, kwa maana hiyo wanahitaji tiba mbadala ili waweze kusherehekea tendo. Wanatakiwa kuboresha mvuto wao katika ndoa au uhusiano na nafasi ya kutekeleza hilo ipo!Ni lazima watu waheshimu uhusiano wao wa kimapenzi. Pia waelewe kwamba moja kati ya vitu vinavyoshikilia penzi lako ni unyumba. Ni wakati muafaka kwako sasa, kuachana na mawazo ya kale. Punguza uvivu na ujue kuwajibika inavyotakiwa, kwa maana ni njia ya kutibu amani yako mwenyewe na mwenzio.

Utafiti unaonesha kwamba asilimia kubwa ya ndoa zinazovurugika kila siku, nyuma yake huwa na shambulio la wanandoa kutopeana huduma ya tendo. Kwamba, wanavumiliana lakini mwisho wa siku, sauti itasikika kwa majirani. Watakapokuwa wanagombezana usiku, siri hugeuka sirini.

Tendo la ndoa, hukamilisha furaha ya wawili walioamua kupendana. Tunapoamua kuacha siasa na kuzingatia ukweli kwa vipimo vyake, watu wengi (hasa wanaume), wanapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, lengo lao la kwanza ni kutimiza haja zao kimwili kwa mtu husika. Nazungumza kwa utafiti!
Walikutana barabarani, akavutiwa ndiyo maana akaanza misele. Anapofanikiwa, vikwazo vya baadaye, inakuwa siyo matarajio yake. Alichotarajia ni kwamba baada ya kukubaliana kuingia kwenye sehemu yenu ‘spesho’, atakuwa hapimiwi! Kwa kiwango chochote atakachokuhitaji, mwenzi wake atamridhia.

Aghalabu, wapenzi ambao wanajikuta wapo kwenye mgogoro wa tendo, mara nyingi hukabiliwa na tatizo la usaliti. Ni theluthi moja ya wanawake wanaoweza kumvumilia mwanaume ambaye hamtoshelezi kimwili, wakati kwa wanaume ni moja ya kumi tu ndiyo wenye kuvuta subira hadi siku watakapokumbukwa.

“Huyu mbona yupo hivi, kila siku anasema kachoka, atakuwa ana mtu huko nje,” ni kauli ambayo ni rahisi kupita kichwani kwa mwanamke, pale ambapo anakabiliana na mwenzi ambaye haguswi chochote na tamaa za mwili, ingawa inaelezwa kwamba ni moja ya kumi ya wanawake ndiyo hukosa usingizi kwa kunyimwa tendo.

0 comments:

Post a Comment