
Hatimaye  Kwa mara ya kwanza staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya  Bongo, Ali Saleh Kiba ameibuka na kumlipua hasimu wake, Nasibu Abdul  ‘Diamond Platnumz’, hali inayotafsiriwa kwamba bifu lao sasa limefika  pabaya ikidaiwa kwamba wanagombea nyota (ustaa).
Kupitia Kipindi  cha The Sporah Show, usiku wa Jumanne wiki hii kwenye CloudsTV, Kiba  alimchakaza Diamond ambapo alifunguka mengi ikiwemo chanzo cha ugomvi  wao. 
Kiba alizungumzia sosi iliyotengeneza bifu kati yake na  Diamond ambapo aliulizwa kama ana namba ya simu ya msanii huyo ndipo  akatiririka:
“Nilikuwa nayo kipindi fulani, nilipohisi amenikosea nikaona sina ulazima wa kuwa nayo.
“Kuna  kipindi alinikosea kwa sababu nilisikia amesema kwamba tulirekodi wote  ule Wimbo wa Single Boy, jambo ambalo halikuwa kweli. Halafu akasema  mimi ndiyo nilimfuta.
“Diamond alinikosea kwa sababu kutokana na  mimi ndiye nilifanya wimbo wake wa Lala Salama ambao upo kwenye album  yake, akanifuta nikahisi amenikosea sana nilichoimba mimi akawa ameimba  yeye, alichoniomba nifanye nilifanya kwa mapenzi yote na mimi namsapoti  kila msanii wa Tanzania anayefanya vizuri, sikatai anaimba vizuri, sijui  ukisema amekopi, mimi sijamaindi wala nini lakini usiseme kwa watu  ukadanganya nikaonekana mimi sifai, siko hivyo mimi.
“Watu  wengine ambao hawaelewi vizuri wanaweza wakamwamini Diamond, kila mtu  ana mapenzi yake labda kuna wengine wanampenda Diamond wengine  wanampenda Ali Kiba. Wanaweza wakawa wengine wanampenda Diamond  wakaamini mimi nilimfuta kwenye wimbo wangu wa Single Boy lakini mimi  wala, shahidi yangu ni produyuza Manecky (AM Records) kwani ndiye  alitengeneza ule wimbo.
“Sikuwahi kwenda studio na Diamond,  sikuwahi kufikiria kufanya wimbo naye. Ila alinipigia simu baada ya ule  wimbo wa Single Boy kuvuja. Akaomba afanye na mimi, akanipa hadi idea  (wazo) ya video, nikamwambia nimeshafanya na Jaydee (Judith Wambura).
"Nikamwambia  itapendeza zaidi tukifanya wimbo mwingine kwa sababu hii tukifanya mimi  na wewe haita-make sense (haitaeleweka), inapendeza ikiwa single boy na  single girl, hicho ndicho kitu nilimjibu.
“Baada ya kama wiki  moja nikasikia kwenye mablog, nikapigiwa simu kwamba mimi nimemfuta  Diamond kwenye ule wimbo wakati yeye ndiye aliyenifuta katika wimbo  wake, shahidi prodyuza wangu KGT.
“Kutoka hapo nikaona hakuna  tatizo lakini kwa kujua yeye alinifuta katika wimbo wake. Mimi siyo  shabiki wa Diamond ni shabiki wa muziki mzuri.
 “Kuna watu  wanasema kachukua kiti changu? Labda kama ni kiti ambacho nilikuwa  nimekaa kina vumbi na ninachotakiwa ni kukipangusa tu na kukaa tena,  labda yeye yuko siti nyingine ila ya nyuma.
“Niliambiwa alisema vitu vingi, mara nilikopa fedha benki ili nimalizie nyumba na mambo kama hayo so siwezi kufanya naye kazi.” 
Baada  ya Kiba kumchakaza, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond naye  alijibu mapigo bila kutaja jina la Kiba ambapo aliandika: “Tatizo  lako wewe unawaza kushindana na mimi ili nishuke…Wakati mwenzako nawaza  kushindana na watu wa mataifa mengine ili nilete sifa na heshima nchini  kwetu.”
Hata hivyo, baada ya hayo yote kuliibuka madai kwamba  mbali na ishu za muziki, mastaa wa kike wa sinema za Kibongo,  Jacqueline Wolper Massawe, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Wema Isaac Sepetu  wanahusishwa kwenye gogoro hilo kisa wivu wa kimapenzi hivyo ishu hiyo  bado ni mbichi






0 comments:
Post a Comment