
Kwa  kawaida kila binadamu anayop siri yake moyoni ambayo hapendi hata siku  moja ifahamike. Lakini kwa upande wa wanaume haijalishi amekuwa na  mahusiano na mwanamke kwa muda gani au amejuana na mwanamke kwa muda  gani hiyo haiwezi kuwa ni kigezo cha kumuamini mpenzi wake kiasi cha  kumweleza siri zake za moyoni. Kuna uwezekano zipo atakazoficha kwa muda  lakini hapo baadaye akaamua kumweleza mwenzi wake, lakini kuna zile  nyingine ambazo nitataja baadhi ambazo kamwe mwanamke asitarajie kuona  mpenzi wake akifungua kinywa chake na kumweleza. Na hata ikitokea  mwanamke akazijua kupitia kwa wapambe, ni dhahiri mwanaume huyo  atakanusha kwa nguvu zake zote na hata aikibidi kutumia ubabe ili kuzima  hoja hiyo..
Kwamba ana matatizo ya kifedha: Inawezekana wakati anakutana na mpenzi  wake mambo yalikuwa safi na alikuwa na fedha za kutosha kula bata na  kuishi maisha ya kifahari, lakini kama ikitokea mambo yakageuka ghafla  bila ya kutarajia kwa mfano alikuwa na njia zake za panya za kupata  fedha nje ya mshahara halafu njia hizo zikafungwa na mshahara ukawa  hautoshi kabisa kukidhi hata robo ya mahitaji yake na mpenziwe, hapo  mwanaume anaweza kutumia mbinu mbalimbali ili kuweka mambo sawa,  ikiwezekana hata kukopa ili kusitiri aibu lakini si kumwambia mpenzi  wake kwamba mambo yamegeuka, labda kama ni mkewe, lakini si mpenzi  ambaye bado mambo hayajaiva
Kwamba aliwahi kubaka au kumla mtungo mwanamke na marafiki zake wakati  fulani: Inawezekana historia yake ya ujana ilikuwa na vibweka vingi  ikiwemo kubaka wanawake au kufanya mapenzi na mwanamke mmoja  akishirikiana na marafiki zake vijana wa mjini huita mtungo au kula  mande. Mwanamke asitarajie mwanaume atafungua mdomo wake na kuelezea huo  upuuzi wake. 
Kukiri kwamba alikudanganganya ili akupate: Kuna wakati mwanaume  hulazimika kudanganya au kuingia na gia kubwa kama vijana wa mjini  wanavyosema ili kumpata mwanamke wa aina fulani. Kuna baadhi ya wanawake  wamejiwekea viwango vya aina ya wanaume watakaopenda watoke nao, shida  ni pale kina Bujibuji watakapokuwa wamefika bei lakini tatizo viwango  viko chini, hapo ndipo mbinu na mikakati vitatumika ikiwezekana kujivika  uhusika asiokuwa nao ili mradi ampate huyo mwanamke, na akimtia  mikononi halafu mwanamke akashtukia kwamba ameingizwa Kingi na kujaribu  kuhoji, asitarajie mwanaume huyo atakiri udhaifu. Lazima atajitahidi  kutafuta namna ya kukwepa kuonekana muongo ili mradi kulinda hadhi yake  ya uongo
Kukiri kwamba aliwahi kufungwa jela na kulawitiwa: Inawezekana mwanaume  aliwahi kufungwa jela, lakini kama inavyojulikana misukosuko ya jela ni  mingi ikiwemo kuingiliwa kinyume na maumbile, au inawezekana mwanaume  katika mazingira fulani aliwahi kuingiliwa kinyume na maumbile kwa  kulazimishwa katika mazingira magumu na ya aibu. Kamwe mwanamke  asitarajie kwamba mwanaume huyu atakuja kufungua mdomo wake na kumweleza  mwanamke kuhusu jambo hilo. hata akija kulisikia mwanaume huyo  atalipinga kwa nguvu zake zote. 
Mwanaume kukiri kwamba alikuwa ANASAFISHA KIWI CHA MACHO: Hata kama  akikamatwa live na mpenzi wake akisafisha kiwi cha macho, si rahisi  mwanaume akubali huo udhaifu, ni lazima atapinga kwa nguvu zake zote.






0 comments:
Post a Comment