Sunday, August 31, 2014

AL-SHABAAB WAMVAMIA ISHA MASHAUZI KENYA......soma hapa kilicho msibu....


Oooh nooo! Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvamiwa na kundi linalojiita Al-Shaabab (siyo wale orijino wanaosifika kwa ugaidi).


Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’.

Tukio hilo ambalo liliibua sintofahamu kwa wananchi, lilitokea juzikati katika hoteli inayojulikana kwa jina la Grassovila iliyopo Mombasa nchini Kenya ambapo walimuibia msanii huyo kila kitu alichokuwa nacho.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Isha alisema kuwa alikwenda Mombasa kwa ajili ya mwaliko wa mashabiki wa Timu ya Arsenal ya England waishio Mombasa na alipokuwa akijiandaa hotelini, ghafla alishtukia watu waliojificha nyuso wakiingia katika chumba alichokuwepo kisha kumuamuru atoe kila kitu.

“Nilishtuka sana kuona kundi la watu likivamia chumbani kwangu, nasikia walianzia katika vyumba vingine, jamaa walinichukulia kila kitu nilichokuwa nacho hadi hati ya kusafiria lakini namshukuru Mungu Watanzania wenzangu walinisaidia na kuweza kurejea Bongo,” alisema Isha.

Alisema polisi nchini humo wanaendelea kufanya uchunguzi kwa ajili ya kuwatia hatiani ‘wahuni’ hao.
Hadi Isha anafanikiwa kurudi Bongo, hakuna mtu yeyote ambaye alikamatwa kuhusiana na tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment