
saa chache baada ya diamond kutangaza ndoa na wema sepetu sasa afunguka na kusema honeymoon itakuwa Dubai na watakaa miezi isiyo pungua Mitatu
 Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na  Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano.  Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo  maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo  yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata  ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani  wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka  tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje  kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi  karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima  uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri,  lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine  kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza  kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba  wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo  Mdogo’ alisema: 
“Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo,  nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu  nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa  haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari,  mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,”  alisema.
Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.
“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati  mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza.
Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: “Hatuna  tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi  kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.
“Lakini ninachoweza kukwambia ni kuwa sisi ndio tunaoujua ukweli wa uhusiano wetu.
“Sidhani kama ni sahihi mapenzi yetu yakawa na wasemaji wengine zaidi yetu wenyewe. Sasa ni ajabu watu wanaposema yao.”






0 comments:
Post a Comment