Ni muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mienendo ya mume wangu kutokana  na tabia yake kubadilika sana siku za hivi karibuni, nikabaini kuwa kuna  msichana anawasiliana naye kwa kutumiana meseji za mapenzi, sikuwa na  haraka nikaamua kufanya uchunguzi wangu kimyakimya”
“Wiki iliyopita mume wangu akiwa amekwenda kuoga akasahau kuzima simu  yake,na siyo kawaida yake kuacha simu yake bila kuizima,mara meseji  ikaingia,nikaangalia nikaona jina la mtumaji amesevu Lulu, moyo  ukalipuka”
Ndivyo alivyoanza kuongea mama mmoja wa makamo anayefanyakazi katika  ofisi moja nyeti katikati ya jiji la Dar alipokuja kuongea na mwandishi  wetu wiki iliyopita baada ya ndoa yake kuingiliwa na mdudu mbaya….
Akiongea kwa masikitiko makubwa, mama huyo ambaye hakupenda kutaja  jina lake kutokana na unyeti wa kazi anayoifanya, alidai kuwa msichana  huyo anayetaka kuiharibu ndoa yake yenye miaka 25 jina lake ni Elizabeth  Michael….
Mama   huyo  alidai  kuwa  jina  hilo  alilibaini  baada  ya  kukuta  meseji   za  mapenzi  kwenye  simu  ya  mume  wake  na  yeye  kuamua   kuifuatilia  namba  hiyo  kwa  kufanya  kama  anataka  kumtumia  pesa   msichana  huyo  na  kukugundua  jina  hilo….
Akiongea   kwa  upole, mama  huyo  alidai  kuwa katika  simu  ya  mume  wake,  jina  la  mtumaji  lilikuwa  Lulu, lakini  alipofanya  uchunguzi  wake   wa  kujifanya  kama anatuma  pesa  kwa  namba  ya  msichana  huyo   ndipo  alipobaini  kuwa  mmiliki  wa  namba  hiyo  ni  Elizabeth   Michael…
Mwandishi   alimuuliza  mama  huyo  kama  anadhani  kuwa  msichana  huyo   anayetaka  kuiharibu  ndoa  yake  ni  muigizaji  maarufu  wa  filamu   hapa  nchini Elizabeth  Michael  “Lulu”, lakini  alikataa  kuthibitisha   hilo  kwa  madai  kuwa  tangu  siku  hiyo  namba  ya  binti  huyo   imekuwa  haipatikani….
“Baada   ya  kugundua  siku  ile ,  nilichukua  simu  yake  na  kutaka   kuwasiliana  naye  ili  niweze  kumuonya  mwenyewe  kimyakimya  kwa   wakati  wangu, wala  sikuwa  na  lengo  la  kuja  kwenye  vyombi  vya   habari , lakini  sikuwahi  kumpata  hewani  tena  kila  nilipojaribu   kumpigia”Alisema  na  kuongeza:
“Huenda   mume  wangu  alishtikia  kuwa  nimeona  ujumbe  ule, kwa  sababu  mimi   nilipoisoma  meseji  ile  sikuifuta, ili  akiona  meseji  imesomwa   aelewe  nimeshajua  kila  kitu, pengine  ndiye  aliyemwambia  binti   huyo  abadili  namba  yake”
Mwandishi   alimuomba  mama  huyo  ampatie  namba  ya  huyo  msichana  ili  kuweza   kujua  kama  ni  Lulu  muigizaji  ama  siyo ( mwandishi  anazijua   namba  zote  za  Lulu ), lakini  namba  hiyo  ni  tofauti  na   anazotumia  Lulu  Mwenyewe….
Mwandishi   alipojaribu  kama  kumtumia  pesa  msichana  huyo, jina  lililotokeza   ni  Elizabeth Michael, na  alipojaribu  kuipiga  namba  hiyo  ilikuwa   haipatikani  hewani….
Juhudi   za  kumsaka  Lulu   ili  kuona  kama  anaitambua  namba  hiyo   hazikuzaa  matunda  kutokana  na  namba  zake  mbili  kutopatikana  na   nyingine  ikiita  bila  kupokelewa….
Angalizo:
Baadhi   ya  wasichana  wa  mjini  wamekuwa  wakitumia  majina  ya  wasanii   maarufu  katika  nyendo  zao  ili  kuwatapeli  watu. Miongoni  mwa   njia  wanazotumia  ni  pamoja  na   kujisajili  kwenye  mitandao  ya   kijamii  kwa  majina  ya  watu  maarufu  ili  kuwatapeli  watu.








0 comments:
Post a Comment