MAPENZI bwana! Baada ya kuogelea kwa muda mrefu katika penzi la muigizaji Kajala Masanja, hatimaye shemeji wa aliyekuwa rafiki wa mwigizaji huyo, Wema Sepetu, Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ ametangaza ndoa na dada wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Abdul.
Kilidai kuwa, Petit alichukua uamuzi huo baada ya kushauriwa na Wema kuwa umri unakwenda na vishawishi ni vingi hivyo ni bora aoe mapema.“Unajua Petit Man anamheshimu sana Wema kwa hiyo alipomwambia Petit kuwa umri unazidi kwenda na anahitaji kuwa na familia yake akaukubali ushauri wake,” kilinyetisha chanzo hicho.
Baada ya kupata maelezo hayo, Ijumaa lilimtafuta Petit Man na kumuuliza kuhusiana na ishu hiyo, bila kuumauma maneno alikiri.“Ni kweli mama (Wema) aliniweka chini na kuniambia kuwa umri unakwenda hivyo nahitaji niwe na familia yangu kwa hiyo siwezi kuwa na familia bila ya kuwa na mke ndipo aliponichagulia mke ambaye ni dada yake wa damu kabisa na Nasibu Abdul ‘Diamond’ anayeitwa Esma na kwa taarifa yako tu, tayari nimeshakamilisha kila kitu,” alisema Petit.
Alipoulizwa kuhusiana na wanawake aliowahi kuwa nao kipindi cha nyuma akiwemo Kajala, Petit alisema huko kote ilikuwa ni njia ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio ambayo ni ndoa yake na Esma.
“Acha nipumzike na madhira ya dunia maana huko kote nilipopita hakukuwa chaguo langu ila kwa Esma nimekufa nimeoza bado kuzikwa tu yaani mimi ni mfu ninayetembea mbele ya Esma.”
0 comments:
Post a Comment